Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 6 YA 31

Tusikubali kamwe unafiki kupata nafasi katika kanisa letu (taz. somo la jana), maana ni kama chachu (au hamira). Kikiingia kidogo tu katika donge la unga kitaenea katika donge lote na kulivimbisha. Onyo: usilionee jina la Yesu haya. Fuata maelekezo ya Yesu anaposema, Kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu (m.8-9)! Faraja: 1. Unafiki utapata hukumu yake. Kwa sababuhakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari (m.2-3)! 2. Tuko chini ya ulinzi wa Mungu mwenyewe. Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope (m.6-7). Kitu kigumu hakiwezi kutendeka maishani mwetu bila ruhusa yake! 3. Watu wanaweza kuuua mwili wetu tu, ila hukumu ya mwisho ni ya Mungu ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum (m.4-5). 4. Mkipata kushitakiwa mbele ya watu msiogope jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema (m.11-12)!

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

https://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha