Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Adui wa MoyoMfano

Enemies Of The Heart

SIKU 3 YA 5

Andy Stanley: Adui za Moyo


Ibada ya Siku ya 3


“Kuacha Maumivu na Hasira”


Maandiko: Waefeso 4:25-32


Adui wa pili ya moyo ni hasira. Tunakasirika wakati ambapo hatupati yale ambayo tunataka.


Nionyeshe mtu aliyekasirika na nitakuonyesha mtu aliyeumia. Na nina uhakika kwamba mtu huyo ameumia kwa sababu kitu kimechukuliwa. Anadai mtu kitu.


Sote twajua watu ambao hasira yao inaweza kusemekana kwa njia mojawapo zifuatazo: “Ulichukua heshima yangu.” “Uliiba familia yangu.” “Ulichukua miaka yangu bora zaidi maishani.” “Uliiba ndoa yangu ya kwanza.” “Ulininyang'anya miaka yangu kama kijana.” “Ulinyang'anya usafi wangu.” “Ninakudai nyongeza.” “Ninakudai fursa ya kujaribu.” “Ninakudai nafasi nyingine.” “Ninakudai upendo.”


Chanzo cha hasira ni mtazamo kuwa kuna kitu ambacho kimechukuliwa. Kuna kitu ambacho unadai. Na sasa uhusiano wa mwenye deni na mwenye kudai umeundwa.


Je wewe? Ni deni lipi linasababisha hasira ambayo unahisi?


Utaruhusu watu ambao wamekuumiza kudhibiti maisha yako kwa muda upi? Mwezi mwingine? Mwaka mwingine? Msimu mwingine wa maisha yako? Muda upi?


Ningependa kupendekeza kwamba leo inafaa kuwa siku ambayo unaacha kushikilia maumivu!


Ingawa ni kweli kwamba huwezi kutengua yaliyokwishatendeka, ni kweli pia kwamba si lazima yaliyopita yadhibiti yajayo. Katika Waefeso 4, tunapewa amri kuwa “tuondoe kabisa uchungu, ghadhabu na hasira.” Tunafanya hivyo kwa “kusameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasemehe ninyi.”


Dawa ya hasira ni msamaha. Ikiwa tutangoja kulipiza kwa maovu yaliyotendwa kwetu, ni sisi tutakaolipa. Ikiwa, kwa upande mwingine, tutafuta deni ambalo tunadai, tutaachiliwa huru.


Kutoka adui hawa wakuu wanne ambao tumekuwa tukijadiliana katika ibada hii, ninaamini ya kwamba hii—hasira isiyotatuliwa inayotokana na maumivu ya kimakusudi ama yasiyokusudiwa—inaangamiza zaidi. Lakini pia ni rahisi kuliko zote kuondokana nayo. Unaamua tu kwamba utafuta deni. Unaamua na kutamka, “Sikudai tena.”


Fuata mchakato huu wenye hatua nne leo: (1) Tambua ni nani ambaye umemkasirikia. (2) Amua unawadai nini. (3) Futa deni kwa kuwasamehe. (4) Usiruhusu hasira ijengeke tena.


siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Enemies Of The Heart

Kama vile moyo unaougua unavyoweza kuangamiza mwili wako, moyo wa kihisia na kiroho unaougua unaweza kukuangamiza pamoja na mahusiano yako. Kwa siku tano zifuatazo, ruhusu Andy Stanley akusaidie kujitazama ndani yako adu...

More

Tungependa kuwashukuru Andy Stanley na Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: bit.ly/2gNB92i

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha