Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Uwezo: Uongozi wa WanafunziMfano

Capacity: Student Leadership

SIKU 1 YA 5

Waefeso 2:10 Hata kabla hujazaliwa Mungu alikuwa na kusudi na mpango kwa maisha yako. Ulikuwa na thamani kwake hata kabla hujafanya chochote. Anataka kukutumia ili kutimiza kusudi hilo na mpango kwa maisha yako. Anza kugundua yale Mungu alikuumba ufanye. Ni kitu gani kinachokupendeza maishani? Ni nini kinachokusisimua? Hiyo inaweza kuwa ishara ya kukuelekeza kwa kile ambacho Mungu anakusudia ufanye na maisha yako. Matendo 9:1-15 Sauli alikuwa na maisha ya kale ya kutisha. Alijitolea kuwatesa na kuwaua Wakristo maisha yake. Lakini Mungu alikuwa na mpango na maisha yake. Mungu aliishia kumtumia Sauli, ambaye baadaye alikuwa Paulo, kueneza ujumbe wa Yesu na amesifika kwa kuandika nusu ya Agano Jipya. Jua ya kwamba maisha yako ya kale hayawezi kuzuia Mungu kukutumia kwa njia ya ajabu. Haijalishi umepitia yepi, umefanya nini, au wewe ni nani; Mungu anaweza na atakutumia. Kwa hivyo, ni vitu gani hivyo ambavyo bado unavishikilia kutoka kwa maisha yako ya kale? Viache viende na uache Mungu asonge.
siku 2

Kuhusu Mpango huu

Capacity: Student Leadership

Mungu anakuitia Mambo Makubwa. Sio tu ukishakuwa mkubwa bali sasa hivi. Mpango huu utakutia moyo na kukuonyesha jinsi ya kuongezeka na muongozo wa unapostahili kuwa maishani sasa hivi. Mungu anaweza na atakutumia kwa nji...

More

We would like to thank Switch, a ministry LifeChurch.tv, for providing this plan. For more information, please visit: www.lifechurch.tv

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha