Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 4 YA 20

Baada ya kubatizwa, Yesu anakwenda nyikani kwa siku arobaini bila chakula. Yesu anarudia safari ya wana wa Israeli ya miaka arobaini nyikani, walikonung'unika na kumwasi Yehova. Lakini ambapo Israeli ilifeli, Yesu anafaulu. Anapojaribiwa, Yesu anakataa kutumia uungu wake kujinufaisha mwenyewe ila badala yake anajihusisha na mateso ya wanadamu. Anamwamini Yehova katika yote na anathibitisha kuwa yeye ndiye atakayebadilisha makosa ya Israeli na wanadamu wote.

Baada ya haya, Yesu anarejea mjini kwao Nazareti. Anakwenda kwenye sinagogi anakoombwa asome Maandiko ya Kiebrania. Anafungua gombo la Isaya, anaisoma na kuketi kisha anaongeza kwa kusema, “Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Waliokuwepo wanashangazwa na wanamkazia macho. Yeye ndiye aliyetabiriwa na Isaya––mtiwa-mafuta anayeleta habari njema kwa maskini, anayewaponya wagonjwa na kuwaheshimisha waliodharauliwa. Yeye ndiye atakayeleta Ufalme wa kinyume na matarajio, ili kurekebisha yasiyofaa na kuufanya ulimwengu kuwa wenye haki tena.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Je, umewahi kushawishika vipi kutumia hadhi na uwezo wako uliopewa na Mungu kujinufaisha au kujionyesha? Fikiria jinsi Yesu alivyomshinda Shetani kwa kutegemea na kukariri maneno ya Mungu. Ni vifungu vipi mahsusi kwenye Biblia vinavyoweza kukusaidia kukumbuka ukweli wa Mungu unapojaribiwa? Vinakili.

•Yesu alitimiza maandiko ya Isaya. Soma Isaya sura ya 61 ukikumbuka hili. Unatambua nini?

•Linganisha jinsi umati unavyopokea habari njema za Yesu katika mstari wa 22 na 29. Je, unapokea vipi ujumbe huu wa Yesu leo?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Mshukuru Yesu kwa kuuchukua uchungu wako na kukuondolea aibu. Mwombe akusaidie ushinde majaribu wiki hii.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video z...

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha