Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

SIKU 1 YA 30

Chakula cha Bwana si kwa kumbukumbu ya mateso ya Yesu tu, bali pia ni tumaini la kuja kwake mara ya pili na tegemeo letu la kuurithi uzima wa milele, kama Yesu alivyosema katika Yn 6:48: Mimi ndimi chakula cha uzima. Ni vema kushiriki, kwani tushirikipo twaonyesha ushirika wetu na Kristo, na kuwa tayari kuokolewa naye kwa njia ya msalaba. Twapokea mwili na damu ya Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhami zetu. Twasoma katika Mt 26:26-28 kwamba Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini ni vema kujihoji kwanza ili kushiriki kwetu kuwe baraka na si laana, maana tushirikipo twatangaza mauti yake msalabani.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Kar...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha