Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoMfano

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

SIKU 1 YA 40




Luka anawahoji mashahidi wengi wa mwanzo waliofahamu maisha ya Yesu, kisha anaandika simulizi ya Yesu. Matukio yenyewe yanaanzia kwenye milima ya Yerusalemu ambako manabii wa kale wa Israeli walitabiri kuwa Mungu mwenyewe atakuja siku moja kuanzisha Ufalme wake kote duniani.

Siku moja katika hekalu la Yerusalemu, kuhani aitwaye Zakaria akiendelea na kazi za ukuhani aliona maono yaliyomshtua. Malaika anamtokea na kumweleza kuwa yeye na mkewe watapata mtoto wa kiume. Hili ni la kustaajabisha kwani Luka anatueleza kwamba Zakaria na mkewe ni wakongwe sana na hawajawahi kupata watoto. Kwa maelezo haya, Luka analinganisha simulizi yao na simulizi ya Abrahamu na Sara, mababu wakuu wa Israeli. Wao pia walikuwa wakongwe sana na hawakuweza kupata watoto hadi pale Mungu kimiujiza alipowapa mwana, Isaka, ambaye kupitia kwake simulizi nzima ya Israeli ilianza. Hivyo hapa Luka anadokeza kuwa Mungu yu karibu kutenda muujiza tena. Malaika anamwambia Zakaria amwite mwanawe Yohana. Anamweleza kwamba mwanawe ndiye aliyetabiriwa na manabii wa kale wa Israeli waliposema kuwa atakuja yule ambaye ataandaa Israeli kukutana na Mungu wao atakapofika kutawala Yerusalemu. Zakaria haamini maneno ya malaika, na anafanywa kuwa bubu mpaka siku Yohana anazaliwa.

Malaika huyo huyo pia anamtokea bikira aitwaye Mariamu na habari kama hiyo ya kushangaza. Yeye pia kupitia muujiza atapata mwana aliyetabiriwa na manabii wa Israeli. Malaika anamwambia amwite mwanawe Yesu na kwamba huyo mwanawe atakuwa mfalme kama Daudi na atatawala watu wa Mungu milele. Anafahamu kuwa Mungu atajivika ubinadamu kwenye tumbo lake na kwamba atamzaa Masihi. Hivyo, japo Mariamu alikuwa msichana wa kawaida tu, anafanywa kuwa mama wa mfalme atakayekuja. Anastaajabu, kisha anaanza kuimba kuhusu jinsi kuinuliwa kwa hadhi yake katika jamii kunaashiria mwamko mkuu zaidi unaokuja. Kupitia mwanawe, Mungu atawashusha watawala kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuwainua masikini na walio wanyenyekevu. Atageuza ukawaida wa mambo ulimwengu mzima.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washi...

More

Tungependa kuwashukuru BibleProject na YouVersion kwa kutupa somo hili. Kwa taarifa za ziada, tafadhalo tembelea: www.bibleproject.com na www.youversion.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha