Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

SIKU 9 YA 31

Kurudi kwa Bwana Yesu kutatanguliwa na ishara ya wazi. Na hatimaye atakapoonekana, vilio vya huzuni kwa waliombeza vitaijaza anga. Hoi hoi za furaha zitasikika kwa waliomwamini. Ni siku ya ajabu wateule watakapokuwa wanakusanywa mbele ya Mfalme Yesu kwa mashangilio makuu. Bwana atuonya tusome sana matukio ya ulimwenguni. Ndiyo yanayotuandaa kuelewa bila mashaka kwamba Mwana wa Mungu yu karibu mlangoni. Nayo yatutosha kujiandaa kumlaki Bwana Yesu badala ya kudadisi tarehe ya tukio hilo; ambayo Mungu ameiweka sirini mwake.

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mun...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha