Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Moyo - Neno La Mungu Hugeuza MoyoMfano

Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo

SIKU 1 YA 5

Neno La Mungu Hugeuza Moyo


Mungu anapo umba dunia pale kwenye hadithi ya Bibilia, tunaona akitumia maneno yanayo angazia yeye jinsi alivyo, ukweli wa bibilia, na miujiza yake. Mara kwa mara, Yesu anatumia maumbile kuwafunza watu. Lengo la hadithi hii ifuatayo ya kiwavi (mdudu) ni kufafanua funzo la bibilia la Mwoyo.


Fikiria kama ungali bado mtoto mchanga kisha unapo cheza upate mdudu wa kiwavi. Kwa furaha, unamchukua yule ndudu na kumweka kwenye chupa iliyo na vijiti na matawi. Unashangaa na kupata raha unapo tazama yule mdudu akitembea mle ndani mwa chupa kwenye makaazi yake mapya.


Siku moja, unampata yule kiwavi (mdudu) kwenye kijiti anakaa ni kama amezirai mle. Baada ya kutazama kwa kina, unaona nyuzi nyeupe zumemzingira. Unashangaa ni nini kinachotendeka? Baada ya siku chache unaanza kupata hofu ukidhania huenda ikawa yule kiwavi amefariki. Baada ya kuangalia kwa kina, unagundua kuna tundu kwenye zile nyuzi zilizo mzingira. Unapo karibia na kutazama zaidi, unaona kuna mdudu tofauti na yule kiwavi anayejaribu kutokea kwenye lile tundu. Unatazama kwa muda mrefu na kustaajabu unapomuona kipepeo mwenye rangi za kupendeza akitokea kwenye lile tundu. Kwa utaratibu, unafungua kifuniko cha ile chupa na kumwona kipepeo akitoka na kupaa hewani.


Unastaajabu na kushangaa, yalitendeka vipi? Miaka nyingi baadae ukiwa kwenye funzo la Bayologia unapata fahamu – yale mabadiliko ya yule kiwavi ilikua ni hali ya maumbile ya kipepeo. Mchakato huo ndio chanzo cha funzo la Mwoyo – “Neno la Mungu hubadili roho.” Neno kubadili linamaanisha kupata umbo jipya, kufanana upya, na kuwa na hali mpya. “Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja " 2 Wakorintho 5:17.


Unaposoma, kuwazia na kufuata Neno la Mungu, mabadiliko ya ajabu yataanza kutendeka kwenye mwoyo wako, sambamba na ule mfano wa kiwavi na kipepeo kwenye zile nyuzi. Mabadiliko haya mwoyoni yataanza kudhihirika katika maisha yako ya kila siku, na kuleta maisha mapya hambayo haungedhani ingeweza kutendeka. Wewe ni kiumbe kipya!


Kila siku: soma maandiko, omba ili ufahamu na ujibu maswali.


Andika ujumbue wa utumaini ,usaidisi,na kuelekezwa kwa mungu anakupa kutokana kwa haya maandiko.



siku 2

Kuhusu Mpango huu

Moyo - Neno La Mungu Hugeuza Moyo

Unaposoma, kuwazia na kufuata Neno la Mungu, mabadiliko ya ajabu yataanza kutendeka kwenye mwoyo wako, sambamba na ule mfano wa kiwavi na kipepeo kwenye zile nyuzi. Mabadiliko haya mwoyoni yataanza kudhihirika katika mai...

More

Tungependa kuwashukuru NBS2GO, Rebecca Davie, na Debbie McGoldrick kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.nbs2go.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha