Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Hatua Zako za MwanzoMfano

Your First Steps

SIKU 2 YA 5

OMBA



Nilisoma darasa la hesabu ambapo tulianza kuzungumza kuhusu algorithimu na coding. Ukitaka kucode computer, lazima uwe na uhakika kabisa. Ili kutusaidia kuelewa, mwalimu alihitaji darasa lieleze, hatua kwa hatua, jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga na sendwich ya jeli.



Ili kufanikiwa, tulitakiwa kupitia katika maumivu makali ya hatua. . .



Fungua kopo la siagi ya karanga.



Fungua mfuniko kwenye meza iliyo pembeni ya kopo la siagi ya karanga.



Chukua kisu cha siagi.



Chovya kisu cha siagi kwenye kopo lililowazi la siagi ya karanga.



Nk., nk., nk.



Kutengeneza sandwich hakutakiwi kuwa jambo gumu!



Wakati mwingine, tunafanya maombi kuwa magumu sana. Kama unamfuata Yesu, kwa hiyo maombi yanatakiwa kuwa sehemu ya mara kwa mara ya maisha yako, siyo kwa sababu ya kazi ya kidini, lakini kwa sababu ya jinsi maombi yalivyo.



Maombi ni mawasiliano; inachukua muda kujieleza kwa Mungu(kwa uwazi) vitu unavyovipitia.



Maombi ni tafakuri; ni kutulia, na kuwa msikivu katika njia nyingi ambazo Mungu anazungumza na kufanya katika maisha yako.



Maombi ni shukrani; ni kuwa na shukrani kwa maisha ambayo Mungu amekupa.



Maombi ni mwelekeo; ni kuyaelekeza maisha yako kufuatana na mapenzi ya Mungu tofauti na mapenzi yetu wenyewe.



Usiyafanye magumu; fanya maombi ukimaanisha. Maombi hayatakiwi kuwa kuchukua muda mrefu, lakini kwa kadri unavyofanya maombi, ndivyo utakavyotamani kuwa na muda zaidi na Mungu.


Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Your First Steps

Umefanya uamuzi wa kumfuata Yesu, sasa nini kinafuata? Mpango huu si orodha kamili ya kila kitu kinachokuja kutokana na uamuzi huo, lakini utakusaidia kuchukua hatua zako za kwanza.

Tunapenda kuwashukuru SoCal Youth Ministries - AG kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea visit: http://youth.socalnetwork.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha