Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 9 YA 14

Mungu Huzungumza Kupitia Kwa Karama na Vipaji


Moyo wa mtu huifikiri njia yake; bali Bwana huziongoza hatua zake (MITHALI 16:9) 


Watu hushangaa na kujiuliza, ninafaa kufanya nini na maisha yangu?  Kusudi la kuwa hai ni lipi? Je, Mungu ana mpango juu ya maisha yangu? Njia moja ambayo Mungu hutumia kujibu maswali haya ni kupitia kwa karama na vipaji vyetu vya kawaida. Hutuongoza kuelewa kusudi letu kupitia kwa ujuzi na vipaji anavyotupatia. 


Kipaji kilichotolewa na Mungu au tunachokiita “karama,” mara nyingi ni kitu tunachoweza kufanya kwa urahisi, kitu ambacho ni kama cha kawaida. Kwa mfano wasanii wengi wa kutajika wanajua jinsi ya kuweka pamoja maumbo na rangi, kwa hivyo hufurahia kupaka rangi, kuchonga sanamu na kusanifu mijengo. Waandishi wengi wa nyimbo husikiza nyimbo katika akili zao na kuandika hizo melodia na/au maneno ili kutunga muziki mzuri. Baadhi ya watu wana vipaji walivyozaliwa navyo vya kupanga au kuongoza, huku wengine wakiwa wamepewa karama za kushauri, kusaidia watu kulainisha maisha yao na mahusiano. Haijalishi karama tulizo nazo, tunapata raha tele kutokana na kufanya kitu tunachojua kufanya bila kujilazimisha.  


Iwapo   hauna hakika na kusudi lako katika maisha, fanya tu kile unachojua na   kufurahia kukifanya kisha umtazame Mungu akithibitisha uteuzi wako kwa   kubariki bidii yako. Usiishi maisha yako ukijaribu kufanya kitu ambacho   hukutunukiwa kufanya. Watu wakifanya kazi ambazo hawakutunukiwa, wanakuwa na   dhiki- na pia wale walio karibu nao. Lakini watu wakiwa mahali pao   panapostahili, watafanikiwa katika kazi zao na kuwa baraka kwa waajiri wao na   waajiriwa wenzao.


Tukifanya   kile ambacho tunajua kufanya, tutahisi upako wa Mungu (uwepo na nguvu) kwenye   bidii zetu. Tutajua kwamba tunatumika katika karama zetu na kwamba kufanya   hivyo kunamtukuza Mungu na kuhudumu maisha kwa wengine. Mungu huzungumza nasi   kupitia kwa upako huu, akitupatia amani na furaha ya kujua kwamba tunatimiza   mpango wake juu ya maisha yetu.


NENO LA MUNGU KWAKO LEO


Fanya unachofurahia kufanya- ni karama ya Mungu kwako wewe.

Andiko

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumis...

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha