Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kutafuta Njia ya Kumrudia MunguMfano

Finding Your Way Back To God

SIKU 2 YA 5

"Ninatamani Ningeanza Upya"





Yafuatayo katika mafanikio yetu katika safari yetu ya kurudi kwa Mungu tunayaita Muamko kwa majuto. Unaangalia maisha yako asubuhi moja na kutambua kuwa, kwa juhudi zako bora zote, umefanya makosa na kuleta fujo katika mambo. Unajazwa na masikitiko na majuto. Na kwa vile sasa unayaona mambo vyema na kwa uwazi zaidi, ungependa kupewa fursa nyingine. Lakini huna uhakika kama utapata.





Lakini, hembu fikiria, mbona upewe fursa nyingine?





Lakini kaa nasi.





Ndani ya kila mmoja wetu kuna thibitisho kuwa tulikuja kutoka kwa uzuri na upendo na kwamba tuliumbwa kupata zaidi ya hayo. Tunapokuwa chini na kutambua fujo na makosa ambazo tumefanya maishani, na kile maisha ya fujo na makosa yametufanya tuwe, tunajibu kwa kusema, "Natamani ningeanza upya tena."





Jambo zuri ni kwamba, unaweza anza upya. Fikira zako kuhusu asili yako katika wema na upendo ni sahihi kabisa. Mungu anakuruhusu kuanza tena upya.





Wengi wetu, wakati tuko tayari kuanza upya tena, tunataka kuyarudia yale maisha tuliyokuwa nayo kabla mambo hayajaharibika. Lakini Mungu ana mawazo mengine. Hataki tu kutusaidia tuyarudie yale maisha mazuri kama tunavyofikiria. Anataka tuwe na maisha tofauti kabisa. Sio tu maisha yako ya baadaye ambayo hubadilika unapomkubali Mungu maishani mwako lakini pia maisha yako ya kale na ya sasa.





Uko tayari kumalizana na msururu wa siku za mateso na maumivu za kale, kukosa madhumuni katika maisha yako ya sasa, na kukosa imani katika maisha yako ya baadaye? Safari yako ya kutoka kwa majuto na kuelekea nyumbani katika Mungu itakuelekeza pia kwa maisha ya kina na ya ukweli—maisha ambayo yanakualika uanze upya leo na uanze kuishi jinsi Mungu alivyotamani ungeishi siku zote . . . daima.





Ingekuwaje kuamini kuwa Mungu anakuruhusu kuanza upya tena leo? Je, mawazo yako kuhusu maisha ya baadaye yatabadilikaje?


Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Finding Your Way Back To God

Je, unatafuta mengi kutoka kwa maisha? Kutaka mengi ni kuwa na hamu ya kumrudia Mungu— popote uhusiano wako na Mungu upo sasa. Sisi sote hushuhudia ishara—au muamko—tunapotafuta kumrudia Mungu. Safari kupitia kwa moja we...

More

Tungependa kuwashukuru Dave Ferguson, Jon Ferguson na Kikundi cha uchapishaji cha WaterBrook Multnomah kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://waterbrookmultnomah.com/catalog.php?work=235828

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha