Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 1 YA 31

Hapa tunaelezwa kuhusu ile imani iliyomfanya Ibrahimu ahesabiwe haki kwamba ilikuwa ya namna gani! Pia twaambiwa ni imani gani inayoweza kutufanya sisi tushinde kesi yetu katika hukumu ya Mungu! Imani ya Ibrahimu ilikuwa imani ya kuamini ahadi ya Mungu, yaani, ahadi yake ya kufanya jambo lisilowezekana kabisa kwa uwezo wa kibinadamu (m.18-22; zingatia kipekee kwamba Ibrahimu aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa... huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki)! Na imani inayotufanya sisi tuhesabiwe haki na Mungu ni imani inayoamini ahadi ya Mungu kuwa kwa kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo dhambi zetu zimeondolewa na mauti imeshindwa. Tutahesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki(m.24-25)!

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha