Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ingia katika KusudiMfano

Step into Purpose

SIKU 1 YA 5

Mpaka umeshindwa kugusa ardhi 



Maono ni muhimu sana kwa ajili ya kuingia katika kusudi. 



Ezekieli 47 inatuambia juu ya mto unaotiririka kutoka hekaluni, kutoka Patakatifu pa Patakatifu (angalia Isaya 6:1-6). Kifungu hiki kina nguvu sana kwa sababu kinaonyesha kuwa kama ukiutafuta utakatifu wa Mungu, bila shaka utapata maono kwa ajili ya kusudi alilonalo kwa ajili yako.



Lakini, kama kifungu kinavyoonyesha, hili halipatikani katika hali ya starehe.



Ezekieli anaendelea kupitia hatua nne tofauti kabla hajawezakuona. Mara nyingi tunamuomba Mungu atufunulie kusudi letu, lakini tunakuwa tayari kuzama kimo cha magoti tuu. Maono aliyoyaona Ezekieli ni ya uzima tele yakitegemezwa na ukaribu na utakatifu wa Mungu (mto, angalia Zaburi 1:1-3). Mambo yanayotupotosha yanatufanya kutokuendelea na kukosa uzima (Ez. 47:11). 



Ukitaka ufasaha na maono sahihi ya kusudi lako, unahitaji kuingia katika uhusiano na Mungu unaopanua mipaka yako. Uhusiano ambao unazama, mahali ambapo miguu yako haigusi kina cha eneo lako la kustarehe. Ni mahali hapo ambapo unasalimisha utawala wako na, badala yake, kujikuta umebebwa naye katika kusudi ambalo lina uzima tele.






Imeandikwa na Candace Tossas


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Step into Purpose

Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapof...

More

Tunapenda kulishukuru kanisa la C3 la Church Sydney Pty Ltd kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea https://www.c3college.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha