Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SITAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SITA

SIKU 3 YA 7

  

YESU APONYA MWANAMKE NA KUFUFUA BINTIYE YAIRO

"40-43 Basi Yesu aliporudi, umati mkubwa wa watu ukampokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea.Kisha mtu mmoja jina lake Yairo, kiongozi wa sinagogi, akaja na kuanguka miguuni mwa Yesu, akimwomba afike nyumbani kwake,kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa."

"Yesu alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana.

43 Katika umati huo alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna ye yote aliyeweza kumponya."

44 Huyo mwanamke akaja kwa nyuma na kugusa upindo wa vazi la Yesu, mara kutokwa damu kwake kukakoma.

45 Yesu akauliza, “Ni nani aliyenigusa?”

Watu wote walipokana, Petro akasema, 

“Bwana, huu umati wa watu unakusonga na kukusukuma kila upande.”

46 Lakini Yesu akasema, “Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka.”

47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Yesu, akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara.

48 Basi Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.”

49 Yesu alipokuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani kwa Yairo, yule kiongozi wa sinagogi, kumwambia,

“Binti yako amekwisha kufa. Usiendelee kumsumbua Mwalimu.”

50 Yesu aliposikia jambo hili, akamwambia Yairo,

“Usiogope, amini tu, naye binti yako atapona.”

51 Walipofika nyumbani kwa Yairo, hakumruhusu mtu ye yote aingie ndani pamoja naye isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, baba na mama wa yule binti.

52 Wakati ule ule watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili ya huyo binti. Yesu akawaambia,

“Acheni kulia. Huyu binti hajafa ila amelala.” 

53 Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa.

54 Yesu akamshika yule binti mkono na kuita,

“Binti, amka!”

55 Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja

Akaamuru apewe kitu cho chote cha kula.

56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Yesu akawakataza wasimwambie mtu ye yote juu ya yale yaliyotukia.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SITA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha