Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TISAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TISA

SIKU 6 YA 7

  

YESU AMFUFUA LAZARO

1 Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania kijiji cha Maria na Martha dada zake.

2 Huyu Maria, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye yule ambaye alimpaka Bwana mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.

3 Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.”

4 Lakini Yesu aliposikia hayo, akasema, “Ugonjwa huu hautaleta mauti bali umetokea ili kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu.”

"5 Pamoja na hivyo, ingawa Yesu aliwapenda Martha, Maria na Lazaro ndugu yao,baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi."

7 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Haya na turudi Uyahudi.”

8 Wanafunzi wake wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?”

9 Yesu akawajibu, “Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wala watembeao mchana hawawezi kujikwaa kwa maana wanaona nuru ya ulimwengu huu.Lakini wale watembeao usiku hujikwaa kwa sababu hakuna nuru ndani yao.”

11 Baada ya kusema haya, Yesu akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”

12 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala usingizi ataamka.”

Hata hivyo, Yesu alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.

14 Kwa hiyo Yesu akawaambia waziwazi, “Lazaro amekufa.Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwepo huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake.”

16 Tomasi aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye.”

17 Yesu alipowasili huko alikuta Lazaro amekwisha kuwako kaburini siku nne.

18 Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu umbali wa karibu maili mbili,

19 Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Maria kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao.

20 Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Maria alibaki nyumbani.

21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.Lakini sasa ninajua kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakupa.”

23 Yesu akamwambia, “Ndugu yako atafufuka.”

24 Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.”

25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi

26 na ye yote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele."Je, unasadiki haya?”

27 Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni.”

28 Baada ya kusema haya Martha alikwenda, akamwita Maria dada yake faraghani na kumwambia, “Mwalimu yuko hapa anakuita.”

"29 Maria aliposikia hivyo, akaondoka upesi akaenda mpaka alipokuwa Yesu.

30 Yesu alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha.

31 Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Maria nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani ya kwamba alikuwa anakwenda kule kaburini kulilia huko.

32 Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa, alipiga magoti miguuni Pake na kusema,

“Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangalikufa.”

"33 Yesu alipomwona Maria akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Yesu alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana.

34 Akauliza, “Mmemweka wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo upaone.”

"35 Yesu akalia machozi. Ndipo Wayahudi wakasema, “Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!”

37 Lakini wengine wakasema, “Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?”

38 Yesu kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa penye ingilio lake. Yesu akasema, “Liondoeni hilo jiwe.” 

Martha ndugu yake yule aliyekuwa amekufa akasema,

"“Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwako kaburini siku nne.”

40 Yesu akamwambia, “Sikukuambia kwamba kama ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”

41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka penye kaburi. Yesu akainua macho yake juu akasema, 

"“Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia.

42 Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya umati huu uliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma.”

43 Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti yake akaita, “Lazaro, njoo huku!”

"44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake.

Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.”

45 Hivyo Wayahudi wengi waliokuwa wamekuja kumfariji Maria, walipoona yale Yesu aliyoyatenda wakamwamini.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TISA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha