Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANEMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

SIKU 7 YA 7

  

MFANO WA MSAMARIA MWEMA

25 Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamwuliza,

“Mwalimu, nifanye nini ili nipate kurithi uzima wa milele?”

Yesu akamjibu, “Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?”

Akajibu,

‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote, tena mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

Yesu akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

Lakini yule mtaalamu wa sheria akitaka kuonyesha kuwa mwenye haki, akamwuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani?”

Yesu akamjibu akasema, “Mtu mmoja alikuwa akitelemka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, naye akaangukia mikononi mwa wanyang'anyi, wakampiga, 

wakaondoka, wakamwacha karibu ya kufa.

Kwa bahati nzuri kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani.

Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipofika mahali pale, alimwona, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani

Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomwona, alimhurumia,

akamwendea, akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga.

Ndipo akampandisha kwenye punda wake akamleta mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza.

Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yo yote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’

“Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu, wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyang'anyi?”

Yule mtaalamu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemhurumia.”

Ndipo Yesu akamwambia, “Nenda, ukafanye vivyo hivyo.”

siku 6

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA NANE

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha