Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Bila UtulivuMfano

Restless

SIKU 1 YA 3

Simu yako inalipuka. Kalenda yako haikamatiki. Orodha ya vitu vya kufanya inaonekana haina mwisho. Akili yako haiachi kwenda mbio. Unapoamka asubuhi, mara unakabiliwa na wasiwasi unaokukabili siku nzima.

Inaonekana kawaida? Zaidi ya huko nyuma, leo hatujatulia. Naweza kuthibitisha kuna sababu tatu zinazochangia kutokutulia kwa wakristo wa leo. Moja, sisi( kama ulimwengu ulivyo) tunatumia muda mwingi katika burudani, mitandao ya kijamii, kwenye apu na michezo, vitu ambavyo vilikusudiwa kutoa uhai badala yake vimekuwa vinatoa uhai. Pili, Hatuna muda "kuingia (malangoni) mwa Bwana kwa shukurani", ikipelekea kutokutosheka na nia ya kutokutoshekana na kukusanya zaidi. Na mwishowe - haya ni changamoto ya mapambano kwa wataaluma wenye tamaa - tunashindwa kupata muda wa kujikumbusha mara kwa mara kuhusu injili na jinsi utambulisho wetu katika Kristo unavyotuweka huru na nia ya kutaka kufanya zaidi.

Inaweza kuonekana kwamba imerahisishwa sana, lakini kama tatizo leyu ni kukosa utulivu, kwa hiyo suluhisho ni kupumzika kutoka kwenye chanzo cha kukosa utulivu. Ili kupata amani na utulivu wa kweli, yatupasa kila siku kuachana na mahitaji ya kazi zetu au ya dunia hii yanayotuondolea utulivu. Yatupasa tuwe na muda wa kumshukuru Mungu kwa alivyotupa, kuliko siku zote kutaka zaidi. Na lazima tubadilishane vitu vinavyotunyonya ( barua pepe, simu janja, nk) na vitu vinavyotupa uhai ( marafiki, familia, neno la Mungu, nk).

Bahati nzuri, Biblia ina mfano wa aina hii ya utulivu: Sabato. Sasa, mpaka miaka michache iliyopita, sabato ilikuwa ni jina kwangu siyo kitendo. Lilikuwa ni jina la kale kwa siku ya juma, siyo kitu ambacho wakristo wa leo wanakifanya. Kwa muda mrefu sabato ilionekana kama ni kitu cha kisheria zaidi kwangu kuliko zawadi ya neema itakayoondoa mahangaiko yangu. Lakini kwa kusoma kwa makini maneno ya Yesu, nimebadirika kabisa jinsi navyoifikiria sabato kama pumziko. Sasa siwezi kufikiria maisha yangu bila hiyo.

Kesho, tutaangalia sabato ni nini kwa wakristo wa leo, kuzama kwa hadithi nyingi ( nilizo au ulizo) ambazo zilishikwa na watu wa zamani. Ndipo, siku yetu ya mwisho katika mpango huu, tutaangalia Biblia inasema nini kuhusu kupumzika siku ya sabato na kwa siku za leo itaonekanaje kwetu

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Restless

"Mioyo yetu haina utulivu mpaka ipate ulivu kwako." Haijawahi kutokea kuwa wengi wetu tukakosa utulivu Agustine alielezea kwa hii sentesi maarufu. Lakini suluhisho kwa kukosa utulivu wa kweli kwetu ni nini? Huu mpango wa...

More

Tungependa kuwashukuru Journey Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.jordanraynor.com/restless/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha