Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Unayo Maombi!Mfano

Unayo Maombi!

SIKU 1 YA 6

“Tunalo la   Kuomba!”


Msemo wa   siku nyingi, “hana la kuomba” unaonyesha mtu ambaye anakabiliwa na hali ya   kutoweza kabisa kufanikiwa. Au mtangazaji wa michezo anaweza kusema, “Aliomba,”   pale ambapo mchezaji anapofunga goli dakika za mwisho tena akiwa mbali kabisa   ya goli na filimbi ya mwisho kulia. 


Lakini   Mungu hakusudii kwamba maisha yetu ya maombi iwe ndio jambo la mwisho la   kushinda magumu baada ya kujaribu njia na rasilimali nyingine. Ukweli ni   kwamba Mungu anataka maombi yawe ni kiini cha maisha ya kila Mkristo: jambo   la kwanza tunaloliendea tunapokuwa na mahitaji, na sio la mwisho. Anataka   kusikia kutoka kwetu katika siku yote, kila siku,  katika wakati tunapokuwa na mahitaji na   katika wakati tuna kila kitu na kutoshelezwa. Pia Mungu anataka kuonyesha   Upendo wake kwa njia nyingi kwa kuwa na mawasiliano ya kudumu na sisi   tunapoomba.


Maombi ni   ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu, ni msingi   wa kutufanya kukua katika mwendo wetu na Mungu. 


“Kuomba   kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” Yakobo 5:16

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Unayo Maombi!

Gundua kanuni ya kujenga maisha ya maombi yenye nguvu na ufanisi. Maombi – mawasiliano na Mungu kwa mtu binafsi – bi ufunguo wa kuona mabadiliko chanya katika maisha na mazingira yetu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwac...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha