Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano

Six Steps To Your Best Leadership

SIKU 5 YA 7

Uhusiano wa Kuanzilisha



Tulianza Mpango huu wa Biblia kwa kukata shauri kuweka kuwa kabla ya kutenda. Ikiwa unataka kubadili wewe ni nani, utahitaji kubadili watu wanaokuzunguka. 



Mtume Paulo, ambaye aliandika vitabu vingi katika Agano Jipya, alipitia badiliko maarufu sana katika Biblia. Badiliko hili katika maisha yake lilikuwa kuu sana hadi jina lake lilibadilishwa kutoka Saulo kuwa Paulo. 



Sauli aliwachukia Wakristo na alitaka wafe. Kisha Paulo akapenda Wakristo kwa maisha yake yote. Sauli alichukua wafuasi wa Yesu na kusafiri kuwawinda. Paulo akakutana na Yesu njiani na kusafiri kuwajulisha watu kumhusu. Sauli alikaa na watu waliomcha Mungu akijaribu kupata njia kumfikia Mungu. Paulo alikaa na watu wapotevu akiruhusu Mungu kufanya njia yake ndani yake.



Kwanza, Paulo alikutana na Yesu ambaye alimwezesha kuelewa mambo. Kisha akakutana na Anania ambaye alimsaidia kupata nguvu mpya na kuona waziwazi (kwa uhalisi). Kisha akakutana na Barnaba, ambaye alimtetea Paulo na kumjulisha kwa viongozi msingi wa Kanisa wakati ambapo bado walimwogopa. Orodha unaendelea na unaweza kusema kwamba leo Paulo ni kiongozi maarufu sana katika historia. 



Kama Paulo, pengine ni uhusiano mmoja tu ambao utabadilisha maisha yako. Ukiamua kukaa na watu, usiitikie tu watu wanaouliza. Anzisha hatua na watu wanaokunyoosha, wanaokusukuma, na hata kukuchanganya akili. 



Jifunze kutokana na Paulo na ukutane na mtu unayemkosoa. Mara nyingi tunahukumu vitu ambavyo hatuelewi. Usikutane tu na watu wa rika lako, wa kazi yako, ama tajriba kama yako. Umekwama? Tafuta mtu aliyekuzidi kidogo. Ikiwa una miaka 30, kutana na mtu wa miaka 40 na umwulize jinsi anavyofikiri tofauti na alipokuwa na miaka 30. 



Jipange kusikiliza mengi, kuuliza maswali mema, na kufuata mifano mema. Usinakili tu vitu ambavyo watu wengine wanafanya, bali jifunze jinsi wanavyofikiri. 



Mwishowe, ikiwa hujaanzisha uhusiano na Yesu, inaelekea kwamaba u uhusiano mmoja kutoka kubadilisha maisha yako. Najua kwamba hiyo ni ukweli maishani mwangu. Maandiko ya mwisho ya leo ni ufafanuzi wa Mtume Paulo kuhusu maisha kama huo. 



Nena na Mungu: Mungu, unajua ni nani ambaye uliniumba kuwa. Unaweza kunisaidia kuona ni nani ninafaa kukutana naye? Nipe hekima na nguvu kutekeleza uhusiano unaofaa.



Utujulishe ikiwa unaamua kuanzilisha uhusiano na Yesu .


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Six Steps To Your Best Leadership

U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusi...

More

Tungependa kushukuru Craig Groeschel na Life.Church kwa ajili ya kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.craiggroeschel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha