Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Tumaini la KrismasiMfano

The Hope Of Christmas

SIKU 1 YA 10

Neno kwa wenye Hekima





Soma leo mistari ya Biblia.





Tazama eneo lolote la kuzaliwa, na kuna uwezekano wa kuona wahusika ambao hawana habari ni nini kinachotendeka: Mamajusi. Tumewazoea, lakini ukiwatazama kwa makini, wanaonekana kutoelewa ni nini kilichotendeka kwa kuvalia nguo za kifahari na kuwa na zawadi zenye dhamana kuu.





Lakini kwangu mimi, mamajusi hao ndio wa kuvutia mno katika hadithi ya Krismasi. Hatujui mengi kuwahusu. Hatuwajui ni kina nani na wala wanatokea wapi. Biblia inawaita "Mamajusi." Mamajusi walikuwa mchanganyiko wa wanafalsafa, wanasayansi na wanafalaki. Walikuwa matajiri na wenye elimu ya juu. Lakini ni hayo tu tunayoyajua kuwahusu.





Lakini tunajua walikuwa wenye hekima. Kwa kweli, tunaweza kujifunza mengi kutoka na hekima wanayoonyesha katika hadithi hii ya Krismasi.





Miongoni mwa masomo kutoka kwa Mamajusi, ni kujifunza kuwa watafuta ukweli. Watu wenye hekima hawana furaha na mambo ya uvumi wala ya kukisia. Wanataka kujua ukweli kumhusu Mungu, maisha yao ya kale na maisha yao ya hapo mbeleni. Mamajusi wakauliza,"Yuko wapi mtoto, philosophers, scientists, and astronomers, Mfalme wa Wayahudi?" (Mathayo 2:2a)





Mamajusi walikuwa wakimtafuta Yesu. Watu wenye hekima wangali wanamtafuta hata leo.





Kuna watu aina mbili maishani katika swala la ukweli: walanguzi na watafutaji. Walanguzi hutengeneza dhana kuhusu ukweli. Walanguzi hudhani wanamjua Mungu alivyo.





Walanguzi wanapenda kuhoji na kumjadili Mungu, lakini ni tetesi tu — kwa sababu hawataki kujua ukweli. Wanataka tu kumwongea.





Kwa upande mwingine, Mungu anapenda wale ambao huchukua muda kutafuta ukweli. Watafutaji hufanya vitu vinne:





• Wanauliza maswali.


• Wanajifunza.


• Wanatazama kinachoendelea karibu nao.


• Wanafanya lolote wawezalo kupata majibu.





Wanamtafuta Yesu kwa vyote walivyonavyo. Mungu anawapenda watafutaji. Biblia inatuambia,"Kisha kutoka humo nchini mtamtafuta Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nanyi mtampata kama mkimtafuta kwa moyo wote na roho yote." (Kumbukumbu la Torati 4:29).





Ukilichukulia swala la kutafuta ukweli kwa uzito, basi huwezi ukaukosa ukweli.





Manake Mungu hataruhusu uukose.
siku 2

Kuhusu Mpango huu

The Hope Of Christmas

Kwa watu wengi, Krismasi imekuwa orodha ndefu ya vitu vya kufanya ambavyo huwaacha wakiwa wamechoka na kutaka Desemba 26 ifike. Katika msururu huu wa jumbe, Mchungaji Rick anataka kukusaidia kukumbuka sababu ya kusherehe...

More

Hii ni Ibada ya 2014 ya Rick Warren. Haki zote zimehifadhiwa. Imetumiwa kwa ruhusa

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha