Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa YesuMfano

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

SIKU 1 YA 7

Bwana Yesu, Najisalimisha kwako.



Kusalimu amri ni semi ngumu kukubali. Kusalimu amri kunaonekana kama kushindwa, na hakuna mtu anataka kuhisi kama ameshindwa. Si ajabu pia kwamba ni ngumu kujisalimisha kwa Mungu. Silika yetu kama binadamu inatuambia kuwa pengine kujisalimisha kwake haitatupa faida. Labda ametukasirikia, ama yamkini tutapoteza maamuzi juu ya tunachotaka. Lakini Maandiko yanatuambia kwamba kujisalimisha kwa Yesu ni njia bora zaidi kwa maslahi yetu.



Mungu amempa Yesu mamlaka kuu na kamili juu ya uumbaji wote. Kupiga magoti, ishara ya unyenyekevu na uaminifu, ni jambo lifaalo kwa mwenye enzi kuu wa ulimwengu. Tunaona uhusiano huu kati ya wafalme au malkia na raia wao. Lakini Yesu akiwa mtawala wetu, tunajua kwamba atatutendea fadhili na upendo mkamilifu, na kwamba mpango wake na Kusudi lake kwa maisha yetu zitakuwa njema daima, hata kama nyakati nyingine ni ngumu na chungu. 



Mungu ametuumba, na ametukomboa na adhabu na utumwa wa dhambi. Alituahidi maisha ya uhuru na kuzaa matunda. Hatuna sababu ya kutetemeka kwa hofu juu ya yale ambayo kujisalimisha kwake kutatuletea. Hakusudii kufanya maisha yetu kuwa ya huzuni, lakini anataka tushiriki katika ufalme ambao umejaa upendo.



Kumfuata Yesu kikamilifu kunahitaji kujisalimisha kwake. Hatuwezi kufuata ajenda yetu wenyewe na wakati huohuo kumfuata. Kujaribu kufanya yote mawili yatatupa mvutano na msongo wa mawazo. Hatujui atakapotuelekeza, lakini tunajua kwamba yeye ni mwema na wa kuaminika. Na alituumba kwa ajili ya matendo mema, aliyotutayarishia.



Sasa ni wakati wa kumpa usukani aongoze maisha yako hadi mahali bora, zaidi ya ulivyojifikiria. 



Siku 6 zifuatazo fungua kila mstari katika sala ya kila siku ya kujisalimisha kwa Yesu ambayo inaweza kubadilisha mwenendo wako na Yesu. 



Bwana Yesu, najisalimisha kwako. 



Kwa nguvu ya Roho yako, nita…



Enda utakapo niende, 



Tenda utakalo nitende, 



Sema utakalo niseme, na 



Toa utakalo nitoe. 



Kwa heshima na utukufu wako. Amina. 






Uko tayari kupiga magoti ili kujisalimisha kwa Yesu awe Mwokozi na Bwana wako?  Ikiwa kuna kizuizi chochote, mwambie kwa maombi, ama uandike barua ukieleza kuhusu kinachokuzuia.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Go Do Say Give: The Freedom Of Surrender To Jesus

Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoel...

More

Tungependa kushukuru Cru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.cru.org/us/en/pledge.html

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha