Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ipe Kazi Yako MaanaMfano

Give Your Work Meaning

SIKU 1 YA 4

Maana ya Kazi Yetu ni Chaguo Letu


Katika Mwanzo 37:5-7 na 9, Yusufu alikuwa na ndoto za wito mkuu ambao Mungu aliweka maishani mwake. Aliota kwamba angekuwa na mamlaka hadi watu wa ukoo wake wangemwinamia. Kaka zake wakamhusudu na kutaka kumwondolea mbali. Walipokuwa mbali na nyumbani na Yusufu akaja kuwajulia hali, wakachukua fursa hiyo na kumwuza katika utumwa. Unaweza kusema, Yusufu alipata kizuizi kikubwa.


Yusufu alilazimika kufanya kazi kama mtumwa katika nchi ya ugeni ambapo watu hawakumheshimu Mungu, lakini hawakuweza kuchukua uhuru wake wa kuchagua mtazamo wake kuhusu kazi yake. Yusufu hakuruhusu cheo chake kuwa utambulisho wake. Japokuwa mkuu wake alikuwa Potifa, Yusufu alichagua kumtumikia Mungu na kufanya kazi yake kwa uhodari. Kwa sababu hiyo, Mungu akampa Yusufu mafanikio katika yote ambayo alifanya, na Potifa akamfanya Yusufu kusimamia mali yake yote.


Wote tuna ndoto za kazi ambazo tunapenda kufanya. Pengine kazi ambayo unafanya sasa hivi haifanani hata kidogo na ndoto ambazo ulikuwa nazo. Hata hivyo, wote tunachagua – kwa kujua ama pasipo kujua – maana ya kazi yetu kwetu. Maana tunayoipa kazi yeti inaongoza mtazamo wetu kuhusu kazi yetu, ambao unaathiri ubora na ufanisi kazini mwetu, na hiyo inaathiri jinsi ambavyo Mungu anaweza kututumia. 


Tuna uhuru wa kuchagua maana chanya ya kazi yetu. Tunapofanya hivyo, kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba tutafanya kazi yetu vyema, na pia tutaruhusu wengine kuona Kristo ndani yetu. Hatimaye, utambulisho wetu ni katika Kristo, wala si kazini mwetu. Muombe Mungu akuonyeshe maana ya kazi yako katika ufalme wake.


Sala


Mungu Baba, nisaidie kuona kazi yangu kupitia macho yako leo. Nisaidie kukumbuka kwamba unatumia kazi yangu yote ambayo nafanya kwa uhodari unaotokana na upendo wangu kwako ili kuonyesha upendo wa Kristo kwa wengine. Naomba wenzangu kazini waone Kristo ndani yangu leo. Katika jina la Yesu. Amina.


Kwa Uchunguzi Zaidi


Gundua jinsi ya kupata maana katika kazi yetu ya kila siku katika  blogu ya Workmatters.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Give Your Work Meaning

Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi n...

More

Tungependa kushukuru Workmatters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:http://www.workmatters.org/workplace-devotions/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha