Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mpango wa Mungu katika maisha yakoMfano

God’s Plan For Your Life

SIKU 2 YA 6

Mpango wa Mungu juu ya maisha yako ni kuhusu wewe ni nani kuliko wewe unaweza kufanya nini.



Nifanye nini? 



Yawezekana umeuliza swali hilo mara nyingi, hasa unapokuwa na jambo la kufanya maamuzi, kama uende chuo gani au uchague taaluma gani. 



Ni swali kama hilo kiongozi wa dini alimuuliza Yesu katika Biblia: Amri iliyo kuu ni ipi?(Matayo 22:36 ) Kwamaneno mengine: nifanye nini?



Katika mstari unaofuata, tunamuona jibu la Yesu : “’Mende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.’ hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’” (Matayo 22:37-39)



Tunapojaribu kufikiria nini mpango wa Mungu maishani mwetu, tunaweza kuanza na mambo haya mawili Yesu aliyotuambia tufanye:



1.) Mpende Mungu.



2.) Wapende watu wengine.



Yawezekana unafikiria, hiyo inaonekana nzuri, lakini nawezaje kujua natakiwa niende chuo gani au taaluma gani nichague? 



Hilo ni swali zuri. Hapa kuna habari njema: Kama unamfuata Yesu na umezungukwa na watu wa Mungu, Roho Mtakatifu atakusaidia kukuongoza katika maamuzi yako.



Unaweza kuwa unachanganywa na vyuo viwili ambavyo vyote vizuri, na unashangaa ni kipi Mungu anataka uende. Hebu turudi nyuma Yesu alisema nini kuhusu amri kuu mbili: kumpenda Mungu na kuwapenda watu. Unaweza kumpenda Mungu na kuwapenda watu katika vyuo vyote viwili? Ikiwa jibu ni ndiyo, basi haijalishi unachagua kipi. Mungu anaweza kukutumia popote.



Inapokuja kwenye maamuzi yetu ya mbeleni, Mungu hatupi majibu ya "ndiyo" au "hapana" siku ote. Hiyo inaweka kuonekana inachangaya, lakini kuna uhuru sana unapotambua Mpango wa Mungu kwa maisha yako n zaidi ya wewe unakuwa nani zaidi ya wewe unafanya nini.



Ina maanisha tunafanya maamuzi yetu wenyewe na kuishi tunavyoaka? Hakika sivyo! tunaweza tusijue mapenzi ya Mungu iku zote, lakini tunaweza kutembea katika njia za Mungu siku zote. Hii ina maana gani? Ina maana kwamba hata kama hatujui kinachofuata katika maisha yetu, tunaweza kuendelea kutii kile ambacho Mungu ametuitia sasa hivi. Ina maana kumfuata, kuishi maisha ya uadilifu, tukitii na kuheshimu wazazi na viongozi wetu, na kumpenda kila mtu Mungu amemuweka maishani mwetu.



Na hapa kuna sehemu bora: Tunapomfuata Kristo, anatupa hekima kupitia Roho Mtakatifu.(1 Wakorintho 2:12-13) Hufanya upya nia zetu (Warumi 12:2) na hutusaidia kutazama mambo yaliyo sahihi. Tunapozungukwa na watu wenye hekima (Mithali 13:20), watatusaidia kufanya maamuzi sahihi, pia. Na moja ya njia bora zaidi tunazoweza kupata hekima ni kupitia maombi. Ukweli Yakobo 1:5 inasema kama tukiomba hekima kwa Mungu, atatupa.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

God’s Plan For Your Life

Je, nini mpango wa Mungu juu ya maisha yako? Ni maswali ya kawaida tuliyonayo wote kama wafuasi wa Kristo. Ila kama tukiwa waaminifu, wazo la mpango wa Mungu katika maisha yetu linaweza kuwa gumu kwetu. Katika siku hizi ...

More

Tungependa kushukuru huduma ya LifeChurch.tv kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.life.church

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha