Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ngumu na Lisa BevereMfano

Adamant With Lisa Bevere

SIKU 1 YA 6


Kwa miaka na mikaka, watu walitafuta kitu ambacho walikiita adamas. Jiwe hili fiche lingekuwa lenye nguvu, lenye sumaku, angavu, na linadumu milele. Viongozi walifikiri kwamba ikiwa wangeweza kulipata, wangeweza kulitumia kuunda silaha na deraya ili kushinda vitani. Kwa miaka na mikaka, mashujaa walienda safari za utafutaji, wakitafuta jiwe hili la ajabu. 


Ninapenda dhana iliyoongoza haya yote. Kuna kitu ambacho kinavutia kuhusu safari za utafutaji na mawe ya nguvu, lakini hakuna mtu anayesafiri akitafuta mawe ya ajabu tena. Wakati huu utafutaji umebadilika. Ulimwengu hautafuti madini yasiyopenyeka tena; unatafuta ukweli usiopenyeka wala kubadilika.


Katika kiini chetu, tunataka kitu thabiti, kitu imara. Hata Pontio Pilato alimwuliza Yesu, “Ukweli ni nini?” Kwa wengi, hili ni swali gumu—na kwa muda mwingi sana, tumekuwa radhi kuliwacha bila jibu.


Tunaishi katika siku ambazo tunahitaji mazungumzo ya kiini, uhusiano wa kiini, fungamano la kiini na Neno la Mungu, ambao ni ukweli. Sisi ni kizazi ambacho kimevuliwa heshima yetu, na mara nyingi tunaachwa na harakati tupu, zinazotupwa na kusukwasukwa mtoni huu uitwao eti ukweli. 


Lakini ukweli si mto. Ni jiwe. 


Na katika mvurugo na ulinganisho huu, sharti tumgeukie Yesu. Yeye ni Jiwe letu, Ngumu yetu: haondoleki wala hatikisiki. Tunaalikwa kufuatisha maisha yetu ndani yake—si tu juu yake, lakini ndani yake—kama msingi wetu imara. Tunapata mali pema pa kusimama kwake pekee katika dunia hii iliyojaa kokoto. 


Tukifanya hivi, anatufanye tuwe imara, kama yeye. Yeye ni jiwe la pembeni, lakini sisi ni mawe yaliyo hai pia, tumejengeka naye ili kuunda nyumba ya kiroho ambayo ni kituo na kimbilio kwa wale ambao wametikiswa na ulimwengu wetu ambao unaendelea kubadilika. 


Hii ni sehemu ya wito wetu kama Wakristo—kusimama imara katika ukweli, si kwa ajili yetu pekee, bali pia kwa ajili ya wale ambao wanatafuta kitu ambacho wanaweza kujengea maisha yao. 


Yesu kuwa Jiwe ina maana gani kwako? Ni katika sehemu zipi ukweli umekuwa katika hali ya kubadilikabadilika ulimwenguni mwako?


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Adamant With Lisa Bevere

Ukweli ni nini? Wanadamu wameanza kuamini uongo kuwa ukweli ni mto, unaopwa na kutiririka na upitaji wa wakati. Lakini ukweli si mto—ni jiwe. Na katika bahari inayochacha ya maoni, mpango huu utakusaidia kutia nanga ya m...

More

Tungependa kuwashukuru John na Lisa Bevere kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://iamadamant.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha