Ufunuo 15:5-6
Ufunuo 15:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya hayo nikaona hekalu limefunguliwa mbinguni, na ndani yake hema ya kuwapo kwa Mungu. Basi, wale malaika saba wenye mabaa saba wakatoka humo hekaluni, wakiwa wamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa na kanda za dhahabu vifuani mwao.
Ufunuo 15:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa; na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung'aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
Ufunuo 15:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa; na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
Ufunuo 15:5-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Baada ya haya nikatazama, nalo hekalu, la hema la Ushuhuda, lilikuwa limefunguliwa mbinguni. Ndani ya lile hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani ingʼaayo na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao.