Zaburi 99:4-6
Zaburi 99:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee mfalme mkuu, mpenda uadilifu! Umethibitisha haki katika Israeli; umeleta uadilifu na haki. Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; angukeni kifudifudi mbele zake. Mtakatifu ndiye yeye! Mose na Aroni walikuwa makuhani wake; Samueli alikuwa miongoni mwa waliomlilia. Walimlilia Mwenyezi-Mungu naye akawasikiliza.
Zaburi 99:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli. Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu. Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia
Zaburi 99:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu; Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili; Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo. Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni penye kiti cha miguu yake; Ndiye mtakatifu. Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake, Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake, Walipomwita Bwana aliwaitikia
Zaburi 99:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa. Mtukuzeni BWANA Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu. Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita BWANA, naye aliwajibu.