Zaburi 91:5-7
Zaburi 91:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Huna haja ya kuogopa vitisho vya usiku, wala shambulio la ghafla mchana; huna haja ya kuogopa baa lizukalo usiku, wala maafa yanayotokea mchana. Hata watu elfu wakianguka karibu nawe, naam, elfu kumi kuliani mwako, lakini wewe baa halitakukaribia.
Zaburi 91:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hutaogopa hatari za usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala mapigo yajayo usiku, Wala maafa yatokeayo adhuhuri, Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako. Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia! Wewe hutakaribiwa na maafa.
Zaburi 91:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.
Zaburi 91:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe.