Zaburi 91:13-16
Zaburi 91:13-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Utakanyaga simba na nyoka, utawaponda wana simba na majoka. Mungu asema: “Nitamwokoa yule anipendaye; nitamlinda anayenitambua! Akiniita, mimi nitamwitikia; akiwa taabuni nitakuwa naye; nitamwokoa na kumpa heshima. Nitamridhisha kwa maisha marefu, nitamjalia wokovu wangu.”
Zaburi 91:13-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Utawakanyaga simba na nyoka, Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu. Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonesha wokovu wangu.
Zaburi 91:13-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Zaburi 91:13-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. BWANA asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu. Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu. Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu.”