Zaburi 77:1-4
Zaburi 77:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Namlilia Mungu kwa sauti, kwa sauti namlilia Mungu anisikie. Wakati wa taabu namwomba Bwana; namnyoshea mikono yangu usiku bila kuchoka, lakini sipati faraja yoyote kwa mtu. Ninamfikiria Mungu na kusononeka; ninatafakari na kufa moyo. Wanizuia hata kupata lepe la usingizi, nina mahangaiko hata kusema siwezi.
Zaburi 77:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia. Katika siku ya taabu yangu nilimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, bila kulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika. Nilipotaka kumkumbuka Mungu nilifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia. Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena.
Zaburi 77:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia. Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika. Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia. Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Naliona mashaka nisiweze kunena.
Zaburi 77:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie. Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika. Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema.