Zaburi 71:4-6
Zaburi 71:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Niokoe, ee Mungu wangu, mikononi mwa waovu, kutoka makuchani mwa wabaya na wakatili. Maana wewe Bwana u tumaini langu; tegemeo langu ee Mwenyezi-Mungu, tangu ujana wangu; nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu, ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu. Mimi nitakusifu wewe daima.
Zaburi 71:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu wangu, uniponye mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu na mdhalimu, Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.
Zaburi 71:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu, mdhalimu, Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu. Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.
Zaburi 71:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee BWANA Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu. Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima.