Zaburi 71:20-22
Zaburi 71:20-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Umenifanya nione taabu nyingi ngumu, lakini utanirudishia tena uhai, wewe utaniinua tena kutoka huko chini. Utaniongezea heshima yangu, na kunifariji tena. Nitakusifu pia kwa kinubi, kwa sababu ya uaminifu wako, ee Mungu wangu; nitakuimbia sifa kwa zeze, ewe Mtakatifu wa Israeli.
Zaburi 71:20-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi. Laiti ungeniongezea ukuu! Urejee tena na kunifariji moyo. Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.
Zaburi 71:20-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Tokea pande za chini ya nchi. Laiti ungeniongezea ukuu! Urejee tena na kunifariji moyo. Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.
Zaburi 71:20-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, utanihuisha tena, kutoka vilindi vya dunia utaniinua tena. Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena. Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze.