Zaburi 71:17-18
Zaburi 71:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, wewe umenifunza tangu ujana wangu; tena na tena, natangaza matendo yako ya ajabu. Usiniache, ee Mungu, niwapo mzee mwenye mvi, hata nivitangazie vizazi vijavyo nguvu yako.
Zaburi 71:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo. Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Zaburi 71:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)