Zaburi 65:6-8
Zaburi 65:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Milima waiweka imara kwa nguvu zako, Huku ukijifunga uweza kama mshipi. Wautuliza uvumi wa bahari, Uvumi wa mawimbi yake, Na ghasia ya mataifa; Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
Zaburi 65:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa nguvu yako uliisimika milima mahali pake. Wewe una nguvu mno! Watuliza mshindo wa bahari na wa mawimbi yake, wakomesha ghasia za watu. Ulimwengu wote washangazwa na matendo yako. Wasababisha furaha kila mahali, toka mashariki hata magharibi.
Zaburi 65:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Milima waiweka imara kwa nguvu zako, Huku ukijifunga uweza kama mshipi. Watuliza kuvuma kwa bahari, Kuvuma kwa mawimbi yake, Na ghasia za watu; Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
Zaburi 65:6-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
uliyeumba milima kwa uwezo wako, ukiwa umejivika nguvu, uliyenyamazisha dhoruba za bahari, ngurumo za mawimbi yake, na ghasia za mataifa. Wale wanaoishi mbali sana wanaogopa maajabu yako, kule asubuhi ipambazukiapo na kule jioni inakofifilia umeziita nyimbo za furaha.