Zaburi 119:174-176
Zaburi 119:174-176 Biblia Habari Njema (BHN)
Natazamia sana uniokoe, ee Mwenyezi-Mungu; sheria yako ndiyo furaha yangu. Unijalie kuishi nipate kukusifu; na maagizo yako yanisaidie. Natangatanga kama kondoo aliyepotea; uje kunitafuta mimi mtumishi wako, maana sikusahau amri zako.
Zaburi 119:174-176 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, Na sheria yako ndiyo furaha yangu. Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu, Na hukumu zako zinisaidie. Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea; Umtafute mtumishi wako; Kwa maana sikuyasahau maagizo yako.
Zaburi 119:174-176 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, Na sheria yako ndiyo furaha yangu. Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu, Na hukumu zako zinisaidie. Nimetanga-tanga kama kondoo aliyepotea; Umtafute mtumishi wako; Kwa maana sikuyasahau maagizo yako.