Zaburi 119:156-158
Zaburi 119:156-158 Biblia Habari Njema (BHN)
Huruma yako ni kubwa, ee Mwenyezi-Mungu, unijalie uhai kama ulivyoahidi. Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Niwaonapo wahaini hao nachukizwa mno, kwa sababu hawazishiki amri zako.
Zaburi 119:156-158 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, rehema zako ni nyingi, Unihuishe sawasawa na hukumu zako. Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini mimi sikiuki shuhuda zako. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako.
Zaburi 119:156-158 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, rehema zako ni nyingi, Unihuishe sawasawa na hukumu zako. Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini sikujiepusha na shuhuda zako. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako.