Zaburi 119:147-149
Zaburi 119:147-149 Biblia Habari Njema (BHN)
Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako. Nakaa macho usiku kucha, ili nitafakari juu ya maagizo yako. Kwa fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, unisikie; unisalimishe kwa uadilifu wako.
Zaburi 119:147-149 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naamka kabla ya mapambazuko na kukuomba msaada, Naweka tumaini langu katika maneno yako. Nakaa macho usiku kucha, Ili kuitafakari ahadi yako. Kwa fadhili zako uisikie sauti yangu, Ee BWANA, uniokoe.
Zaburi 119:147-149 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kutangulia mapambazuko naliomba msaada, Naliyangojea maneno yako kwa tumaini. Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku, Ili kuitafakari ahadi yako. Uisikie sauti yangu sawasawa na fadhili zako, Ee BWANA, unihuishe sawasawa na hukumu yako.
Zaburi 119:147-149 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako. Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee BWANA, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.