Zaburi 119:115-117
Zaburi 119:115-117 Biblia Habari Njema (BHN)
Ondokeni kwangu, enyi waovu, ili nipate kushika amri za Mungu wangu. Uniimarishe ulivyoahidi, nami nitaishi; usikubali niaibike katika tumaini langu. Unitegemeze, niwe salama; niwe daima msikivu kwa masharti yako.
Zaburi 119:115-117 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu. Unitegemeze kulingana na ahadi yako, nikaishi, Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu. Unisaidie nami nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima.
Zaburi 119:115-117 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu. Unitegemeze sawasawa na ahadi yako, nikaishi, Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu. Unisaidie nami nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima.
Zaburi 119:115-117 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu! Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa. Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako.