Zaburi 119:110-112
Zaburi 119:110-112 Biblia Habari Njema (BHN)
Waovu wamenitegea mitego, lakini sikiuki kanuni zako. Maamuzi yako ni riziki kubwa kwangu milele; hayo ni furaha ya moyo wangu. Nimekusudia kwa moyo wote kufuata masharti yako milele.
Zaburi 119:110-112 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Watendao uovu wamenitegea mtego, Lakini sitoki katika njia ya mausia yako. Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu. Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, Daima, naam, hata milele.
Zaburi 119:110-112 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Watendao uovu wamenitegea mtego, Lakini sikuikosa njia ya mausia yako. Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu. Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, Daima, naam, hata milele.