Zaburi 118:5-7
Zaburi 118:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Katika taabu yangu nilimwomba Mwenyezi-Mungu, naye akanisikia na kuniweka huru. Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini? Mwenyezi-Mungu yuko nami, kunisaidia; nami nitawaona maadui zangu wameshindwa.
Zaburi 118:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika shida yangu nilimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wakiwa wameshindwa.
Zaburi 118:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika shida yangu nalimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
Zaburi 118:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia BWANA, naye akanijibu kwa kuniweka huru. BWANA yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? BWANA yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa.