Methali 9:6-9
Methali 9:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.” Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi, amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa. Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia; mwonye mwenye hekima naye atakupenda. Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima; mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.
Methali 9:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu. Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu
Methali 9:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu. Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu. Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu
Methali 9:6-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. “Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi. Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda. Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika.