Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 9

9
Karamu ya Hekima
1 # Mt 16:18; Efe 2:20; 1 Tim 3:15; Ebr 3:3-6 Hekima umeijenga nyumba yake,
Amezichonga nguzo zake saba;
2Amechinja nyama zake, umechanganya divai yake,
Ameiandalia meza yake pia.
3 # Mt 22:3,4,9; Lk 14:17; Rum 10:15 Amewatuma wajakazi wake, analia,
Mahali pa mjini palipoinuka sana,
4 # Mit 6:32; Mt 11:25 Kila aliye mjinga na aingie humu.
Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,
5 # Wim 5:1; Isa 55:1; Mt 26:26-28 Njoo ule mkate wangu,
Ukanywe divai niliyoichanganya.
6Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi,
Mkaende katika njia ya ufahamu.
7Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha;
Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.
8 # Mt 7:6; Zab 141:5 Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia;
Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.
9 # Mt 13:12 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima;
Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
10 # Ayu 28:28; Zab 111:10; Mit 1:7 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima;
Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.
11 # Mit 10:27 Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa;
Na miaka ya maisha yako itaongezwa.
12 # Ayu 35:6,7 Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako;
Na kama una dharau, utaichukua peke yako.
13Mwanamke mpumbavu hupiga kelele,
Ni mjinga, hajui kitu.
14Hukaa mlangoni pa nyumba yake,
Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka,
15Apate kuwaita wapitao njiani,
Waendao moja kwa moja katika njia zao.
16Kila aliye mjinga na aingie humu.
Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,
17 # Mit 20:17 Maji yaliyoibiwa ni matamu,
Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza.
18Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo;
Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 9: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha