Methali 2:4-7
Methali 2:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)
ukiitafuta hekima kama fedha, na kuitaka kama hazina iliyofichika; hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu, utafahamu maana ya kumjua Mungu. Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi, yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu.
Methali 2:4-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu
Methali 2:4-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu
Methali 2:4-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, ndipo utakapoelewa kumcha BWANA na kupata maarifa ya Mungu. Kwa maana BWANA hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama