Mathayo 15:29-30
Mathayo 15:29-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu alitoka hapo akaenda kando ya ziwa Galilaya, akapanda mlimani, akaketi. Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
Mathayo 15:29-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko. Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya
Mathayo 15:29-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)