Walawi 19:35-37
Walawi 19:35-37 Biblia Habari Njema (BHN)
“Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. Ni lazima mtumie mizani halali, na vipimo vilivyo halali. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
Walawi 19:35-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA.
Walawi 19:35-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi BWANA.
Walawi 19:35-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa halali, na hini halali. Mimi ndimi BWANA Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri. “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi BWANA.’ ”