Walawi 16:5-8
Walawi 16:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Atatwaa kutoka jumuiya ya watu wa Israeli beberu wawili kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. “Aroni atamtoa huyo fahali sadaka ya kuondoa dhambi kwa ajili yake mwenyewe, na kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na jamaa yake. Kisha, wale beberu wawili atawaweka kwenye mlango wa hema la mkutano. Atawapigia kura hao beberu wawili, kura moja kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu na nyingine kwa ajili ya Azazeli.
Walawi 16:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi wawili wa kiume, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo dume kwa sadaka ya kuteketezwa. Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.
Walawi 16:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. Na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.
Walawi 16:5-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Atachukua mbuzi dume wawili kutoka kwa jumuiya ya Israeli kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. “Aroni atamtoa huyo fahali kwa ajili ya sadaka yake ya dhambi ili afanye upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na nyumba yake. Kisha atawachukua wale mbuzi dume wawili na kuwaleta mbele za BWANA kwenye ingilio la Hema la Kukutania. Aroni atapiga kura kwa ajili ya hao mbuzi wawili, mmoja kwa ajili ya BWANA na mwingine kwa ajili ya kubebeshwa dhambi.