Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Law 16

16
Sikukuu ya Upatanisho
1 # Law 10:1,2 BWANA akasema na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni, walipokaribia mbele za BWANA, wakafa; 2#Ebr 6:19; Kut 30:10; Law 23:27,28; Ebr 9:7; 10:19; Kut 25:22; 40:34; 1 Fal 8:10-12BWANA akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema. 3#Ebr 9:7-25; Law 4:3Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ng’ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. 4#Kut 28:39; Law 6:10; Eze 44:17; Flp 2:7; Ebr 2:14; Zab 93:5; Kut 30:20; Ebr 10:22Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa. 5#Law 4:14; Hes 29:11; 2 Nya 29:21; Ezr 6:17; Eze 45:22Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. 6#Law 9:7; Ebr 5:1,2; 7:27,28Na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. 7Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. 8Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. 9#Mit 16:33Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya BWANA, na kumtoa awe sadaka ya dhambi. 10#Isa 53:4-10; Ebr 7:26; 9:23,24; Rum 3:25; 2 Kor 5:21; 1 Yoh 2:2Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za BWANA ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli.
11Na Haruni atamsongeza ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake. 12#Law 10:1; Hes 16:18; Ufu 8:5; Kut 30:34; 31:11; 37:29; Ufu 8:3,4Kisha atatwaa chetezo kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za BWANA, na konzi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia. 13#Kut 31:7,8; Hes 16:7,18,46; Ufu 8:3,4; 1 Tim 6:16; Kut 25:21,22Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za BWANA, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. 14#Ebr 10:4Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba. 15#Ebr 2:17; 6:19; 9:12Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ng’ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema, 16#Kut 29:36naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao. 17#Lk 1:10Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli. 18#Ebr 9:22Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za BWANA na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote. 19#Eze 43:20Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke.
20 # Eze 45:20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. 21#Isa 53:6Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 22#Zab 103:1-13; Mt 8:17; Yn 1:29; Ebr 9:28; 1 Pet 2:24Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani. 23#Eze 44:19; 42:14; Flp 2:6-11Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo; 24naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu. 25#Kut 29:13; Law 4:10Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. 26#Law 15:5; Ebr 9:10Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika marago. 27#Ebr 13:11; Law 8:17; 4:12; 6:30Na yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao. 28Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia maragoni.
29 # Law 23:26-32; Hes 29:7-11; Kut 30:10; Isa 58:3,5; Dan 10:3,12 Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu. 30#Eze 36:25; Yer 33:8; Tit 2:14; Efe 5:26; Ebr 9:13,14; 1 Yoh 1:7,9Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA. 31#Kut 31:15; 35:2; Law 23:32; 25:4Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele. 32#Kut 29:29; Hes 20:26Na kuhani atakayetiwa mafuta na kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani, yale mavazi matakatifu. 33Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili ya madhabahu; naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko. 34#Law 23:31; Hes 29:7; Kut 30:10; Ebr 9:7,25Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa.

Iliyochaguliwa sasa

Law 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha