Yobu 37:1-4
Yobu 37:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kutokana na hayo, moyo wangu unatetemeka, na kuruka kutoka mahali pake. Sikilizeni ngurumo ya sauti ya Mungu, na mvumo wa sauti kutoka kinywani mwake. Huufanya uenee chini ya mbingu yote, umeme wake huueneza pembe zote za dunia. Ndipo sauti yake hunguruma, sauti ya Mungu hunguruma kwa fahari na muda huo wote umeme humulikamulika.
Yobu 37:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Moyo wangu hutetemeka kwa hayo pia, Nao huruka kutoka mahali pake. Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake. Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi. Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Yobu 37:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Moyo wangu hunitetema kwayo pia, Nao hutoka mahali pake. Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake. Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi. Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
Yobu 37:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kwa hili moyo wangu unatetemeka, nao unaruka kutoka mahali pake. Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake. Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote na kuupeleka hata miisho ya dunia. Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. Wakati sauti yake ingurumapo tena, huuachilia umeme wake wa radi.