Yobu 36:11-14
Yobu 36:11-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakimtii Mungu na kumtumikia, hufanikiwa katika siku zao zote; miaka yao yote huwa ya furaha. Lakini wasipomtii, huangamia kwa upanga, na kufa kwa kukosa akili. “Wasiomcha Mungu hupenda kukasirika, hawamlilii msaada anapowabana. Hufa wangali bado vijana, maisha yao huisha kama ya walawiti.
Yobu 36:11-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha. Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, Nao watakufa pasipo maarifa. Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira Hawalilii msaada hapo awafungapo. Wao hufa wakingali vijana, Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.
Yobu 36:11-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama wakisikia na kumtumikia, Watapisha siku zao katika kufanikiwa, Na miaka yao katika furaha. Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga, Nao watakufa pasipo maarifa. Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira Hawalilii msaada hapo awafungapo. Wao hufa wakali vijana, Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.
Yobu 36:11-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu. Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa. “Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada. Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.