Yohane 4:13-14
Yohane 4:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu akamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uhai na kumpatia uhai wa milele.”
Yohane 4:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Yohane 4:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.