Yeremia 51:9-10
Yeremia 51:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni. Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia. Twendeni Siyoni tukatangaze matendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Yeremia 51:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni. BWANA ameitokeza haki yetu; Njooni, tutangaze katika Sayuni Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.
Yeremia 51:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni. BWANA ameitokeza haki yetu; Njoni, tutangaze katika Sayuni Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.
Yeremia 51:9-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“ ‘Tungemponya Babeli, lakini hawezi kuponyeka; tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe, kwa kuwa hukumu yake inafika angani, inapanda juu hadi mawinguni.’ “ ‘BWANA amethibitisha haki yetu; njooni, tutangaze katika Sayuni kitu ambacho BWANA Mungu wetu amefanya.’